Ifahamu Kweli: Mafundisho Sahihi ya Neno la Mungu Tanzania
Tunafundisha kweli ya Neno la Mungu ili ikuweke huru.
“Tena mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru.” — Yohana 8:32
Kwanini Tuko Hapa?
Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na wimbi kubwa la mafundisho potofu nchini Tanzania. Kama inavyoonywa katika Mathayo 24:24 na 12:39, jamii nyingi zimejikita katika kutafuta ishara na miujiza badala ya msingi sahihi wa kiroho. Hii imesababisha watu wengi kupotezwa na manabii wa uongo, na hatimaye kupoteza mwelekeo wa maisha yao.
Kila mtu ana hiari ya kuamini anachotaka, lakini lengo letu ni kukusaidia kufanya maamuzi sahihi. Tunajitahidi kukufundisha jinsi ya kutofautisha kweli na uongo kwa kusimama kwenye msingi wa Neno la Mungu. Ahadi yetu katika Kristo ni moja: kukufundisha kweli yote itakayokuletea uhuru wa kweli katika maisha yako ya kila siku.
Dira na Dhima
Dira Yetu (Vision)
Kuwafikia Watanzania zaidi ya milioni 10 na kweli ya Neno la Mungu, ili kujenga jamii iliyo salama na imara kiroho katika nyakati hizi.
Dhima Yetu (Mission)
Kufundisha kweli kwa kila Mtanzania kupitia njia rahisi na zinazoeleweka, ili kweli hiyo imweke huru kiroho na kimwili.
Misingi Inayotuongoza
Ukweli
Tunasimama kwenye kweli ya Neno la Mungu bila kuyumbishwa.
Hofu ya Mungu
Tunaongozwa na staha na utii kwa Mungu.
Ujuzi wa Neno
Tuna uelewa wa kina na sahihi wa maandiko.
Moyo wa Kusaidia
Tuna nia ya dhati ya kuelimisha na kunyanyua jamii.
Kuwa Sehemu ya Huduma Hii
Tuungane Mtandaoni
Tunajenga Huduma Hii Pamoja
Lengo letu ni kuwafikishia Watanzania makala na video zenye ukweli na manufaa kila siku. Ili kufanikisha hilo, tunaendelea kuboresha vifaa na miundombinu yetu ya kiteknolojia. Kila mchango wako unatusaidia kuharakisha kazi hii na kuwafikia watu wengi zaidi.
Saidia Ujumbe Uwafikie Wengi
Shirikisha makala na video zetu kwa ku-share kwenye mitandao ya kijamii. Share yako inaweza kumfikia mtu anayehitaji ujumbe huu leo.
Kadiri unavyoshirikisha, ndivyo watu wengi zaidi wanavyopata tumaini, maarifa na mabadiliko. Asante kwa kuwa sehemu ya kueneza ujumbe huu.
Shirikiana Nasi Kueneza Neno la Mungu
Una ujuzi wa teknolojia, uhariri wa video, au matumizi ya vifaa vya kidijitali? Vipaji vyako vinaweza kusaidia huduma hii kufikia watu wengi zaidi.
Je, una masomo mazuri ya Neno la Mungu ambayo ungependa Watanzania wayasome? Usiyaweke kwako pekee.
Yashirikishe kupitia makala au mafundisho yenye ukweli na manufaa. Mchango wako unaweza kubadili maisha ya wengi.
Saidia Huduma Hii Iendelee
Mchango wako unasaidia kuendesha tovuti hii na kufanya maudhui yaendelee kupatikana bure kwa kila mtu.
Njia za Kuchangia
🟢 Mixx by Yas
📱 +255 656 779 726
👤 NOEL GIPSON MINJA
🟡 Lipa kwa Mixx by Yas
🔢 224663407
👤 NOEL GIPSON MINJA
Hakuna kiwango cha chini cha kuchangia. Toa kile unachoweza kwa moyo wa hiari.
