Ifahamu Kweli: Mafundisho Sahihi ya Neno la Mungu Tanzania

Tunafundisha kweli ya Neno la Mungu ili ikuweke huru.

“Tena mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru.” — Yohana 8:32

Kwanini Tuko Hapa?

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na wimbi kubwa la mafundisho potofu nchini Tanzania. Kama inavyoonywa katika Mathayo 24:24 na 12:39, jamii nyingi zimejikita katika kutafuta ishara na miujiza badala ya msingi sahihi wa kiroho. Hii imesababisha watu wengi kupotezwa na manabii wa uongo, na hatimaye kupoteza mwelekeo wa maisha yao.

Kila mtu ana hiari ya kuamini anachotaka, lakini lengo letu ni kukusaidia kufanya maamuzi sahihi. Tunajitahidi kukufundisha jinsi ya kutofautisha kweli na uongo kwa kusimama kwenye msingi wa Neno la Mungu. Ahadi yetu katika Kristo ni moja: kukufundisha kweli yote itakayokuletea uhuru wa kweli katika maisha yako ya kila siku.

Dira na Dhima

Dira Yetu (Vision)

Kuwafikia Watanzania zaidi ya milioni 10 na kweli ya Neno la Mungu, ili kujenga jamii iliyo salama na imara kiroho katika nyakati hizi.

Dhima Yetu (Mission)

Kufundisha kweli kwa kila Mtanzania kupitia njia rahisi na zinazoeleweka, ili kweli hiyo imweke huru kiroho na kimwili.

Misingi Inayotuongoza

Ukweli

Tunasimama kwenye kweli ya Neno la Mungu bila kuyumbishwa.

Hofu ya Mungu

Tunaongozwa na staha na utii kwa Mungu.

Ujuzi wa Neno

Tuna uelewa wa kina na sahihi wa maandiko.

Moyo wa Kusaidia

Tuna nia ya dhati ya kuelimisha na kunyanyua jamii.

Kuwa Sehemu ya Huduma Hii

    Tuungane Mtandaoni

    FaceBook

    Jiunge na jumuiya yetu kupata habari, makala, na mijadala ya kila wiki.

    Youtube

    Pata mafundisho ya video kila wiki yanayokusaidia kukuza ufahamu wako.